Monday, September 2, 2013

Bale Ndani ya Real Madrid Leo Hii

Hatimaye Gareth Bale amejiunga rasmi na Real Madrid ya Uhispania kwa kuvunja rekodi iliyowekwa na Cristiano Ronaldo.   Jumatatu ya leo imekua ya furaha kubwa ndani ya Jiji la Real Madrid mara baada ya kuwasili kwa mchezaji ghali duniani Gareth Bale akitokea club ya Tottenham ya nhini Uingereza. Amekua mchezaji ghali duniani mara baada ya uhamisho wake kugharimu £86 million (€100 million) kwa mujibu wa Tottenham, ingawa Real Madrid wanadai ni kiasi cha €91million. 
Kiwango kilichotajwa na Real Madrid kinaonekana kuwa ni kwaajili ya kukwepesha ukweli wa rekodi iliyovunjwa na Gareth Bale, ili rekodi ya Cristiano Ronaldo ionekane haijavunjwa bado. Ila ukweli ni kwamba Bale kaivunja rekodi hiyo na ndie mchezaji ghali zaidi duniani kwa sasa.  

PICHA MBALIMBALI ZA DIAMOND KATIKA NYIMBO YAKE MPYA YA NUMBER ONE

Msanii wa kizazi kipya Naseeb Abdul aka Diamond Platinum jana alizindua video ya wimbo wake mpya 'Number One' kwenye hoteli ya kifahari 'Serena Hotel' iliyopo jijini Dar es Salaam.









Add caption