Thursday, August 29, 2013

Msanii Wa Filamu Anusurika Kifo

MSANII wa filamu za Kibongo, Prisca Tadei hivi karibuni alinusurika kifo baada ya kupata ajali mbaya ya pikipiki wakati alipokuwa akielekea ‘location’ kushuti.









Mariamu Athuman ‘Kalunde’ alisema anamshukuru Mungu kwa kuwa msanii wake huyo mpaka sasa anapumua na anaonesha matumaini kwani ilikuwa ajali mbaya.













Ajali hiyo ilitokea wiki iliyopita maeneo ya Mbagala, jijini Dar ambapo Prisca aliumia vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake baada ya pikipiki aliyokuwa amepanda kugongwa na gari ambapo alikimbizwa Hospitali ya Mnazi Mmoja na kulazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu.






Homa la Pambano la Mabondia Cheka na Phil Williams lazidi Kupamba Moto

Bondia wa Marekani `Phil Williams` Atua Dar Kumkabili bondia wa Tanzania Francis Cheka siku ya kesho katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar Es Salaam

Wednesday, August 28, 2013

Jana mchana mwanadada Elizabeth Michael alifanya shopping maalumu ya nguo na vitu vingine kwa ajili ya uzinduzi wa filamu yake mpya ya Foolish Age inayotarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho kwenye ukumbi wa mlimani city jijini Dar es Salaam.

Uzinduzi wa filamu hii ambayo lulu mwenyewe anasema kuwa itakuwa ya kihistoria na aina yake utasindikizwa na wasanii mbalimbali wa kizazi kipya akiwema mwanadada Lady Jay dee.
Baada ya shopping hiyo mwanadada lulu pamoja na mama yake mzazi walipata nafasi ya kufanya mahojiano na kituo cha luninga cha DTV yote ni katika kuizungumzia filamu hii mpya inayotarajiwa kutingisha soko la filamu Tanzania

Hood lagonga mmoja,15 majeruhi

Mtu mmoja amefariki dunia na 15  wamejeruhiwa baada ya basi  la Kampuni ya Hood  likitokea kilombero kwenda jijini  Dar es salaamkumgonga  mtembea kwa miguu na kisha kuacha njia na kupinduka katika eneo la Kiembeni  Mikese Mkoani  Morogoro.
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Morogoro  Bonifasi Mbao  akizungumza kwenye  eneo la tukio amesema chanzo cha ajali  hiyo ni mwendo kasi ambapo dereva wa basi  gari  ilimshinda na kugonga mtembea kwa miguu na kisha kupinduka ambapo  dereva wa basi amekimbia mara baada ya tukio la ajali
Taarifa za  madaktari  katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro  zimeeleza  majeruhi wanaendelea na matibabu na mwili wa marehemu umehifahiwa katika chumba cha maiti hospitali ya mkoa wa morogoro .

KING CRAZY GK ARUDI TENA

Aunty Ezekiel Apigwa Chupa Club Billicanas

Akiwa kitandani
Jumapili iliyopita katika ukumbi wa bilicanas mwanadada, Aunty Ezekiel alipigwa chupa na kujeruhiwa vibaya na mwanadada aliyetambuliwa kwa jina la Ivony Bigirwa katika show ya muziki ambapo wasanii wa muziki wa kizazi kipya waliopo chini ya kampuni  ya Wema Sepetu ya Endless fame walikuwa wakitambulisha nyimbo zao mpya
Chanzo nini?
Baada ya kufuatilia kwa karibu na kuichunguza habari hii bongomovies tumegundua kuwa chanzo kilikuwa ni ‘beef’ la kugombania mwanaume ambaye anasadikika ni mume wa mtu kati ya mwanadada huyo (Ivony) na Aunty Ezekiel
Ilikuaje?
Mpashaji wa habari hii anasema kuwa wanadada hao walikuwa ukumbini hapo na ghafla mwanaume huyo aliyetambuliwa kwa jina moja la Sunday alitokea ukumbini hapo na ndipo patashika hilo likazuka kila mmoja akidai kuwa jamaa huyo ni wa kwake.
Baada ya vuta nikuvute ndipo uzalendo ukamshinda mwanadada ivony na kuanza kuzichapa na Aunty kabla ya kuamua kuchukua chupa na kumpiga nayo na kumjeruhi maeneo ya mkononi
Hali ya Aunty Ezekiel
Kwa sasa hali yam dada huyu iko vizuri na mpaka tunavyoripoti sasa, habari zinasema amesharuhusiwa kutoka hospitalini kwenda kupumzika nyumbani

BABA mzazi  ame
jikuta akiingia matatani mara baada ya kumsababishia majeraha kadhaa mwanaye a kike wakati akijaribu kumtibu ugonjwa wa FANGASI ambao ulikuwa ukishambulia ngozi ya binti wake huyo kwa kiasi kikubwa cha mwili....Akiongea na chanzo chetu cha karibu baba mzazi huyo ambaye hakutaka jina lake kutajwa alisema kuwa alifikia uamuzi huo mara baada ya kuona afya ya Ngozi ya mtoto wake huyo ikidorora siku hadi siku kutokana na maradhi hayo ya ngozi ambayo yalikuwa yamesababishwa na FANGASI ambao walikuwa wameiharibu Ngozi ya mtoto huyo kwa kiasi kikubwa."Nilichemsha maji ya moto na kumuamuru mwanangu angie humo kwani niliona kuwa ndio njia pekee ya kulitibu tatizo hilo kwasababu ametumia dawa nyingi za kienyeji lakini hazikumsaidia kabisa"... alisema baba mzazi huyo  Baada ya kupata majeraha hayo mtoto huyo kwa sasa yupo chini ya Uangalizi wa madaktari Bingwa kwaajili ya matibabu zaidi, lakini mpaka sasa hakuna chombo chochote cha sheria kilichooneshania ya kumshtaki mzazi wa mtoto huyo kutokana na hilo ambalo amelifanya. 

Tuesday, August 27, 2013

VIGOGO WASHIKILIWA NA MALI ZAO

Na Waandishi Wetu
VIGOGO 111 wanaosadikiwa kujihusisha na biashara yharamu ya madawa ya kulevya nchini wameanza kuonja 'joto ya jiwe' kufuatia Jeshi la Polisi Tanzania Kitengo cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola kukamata mali zao, Uwazi lina mpango mzima.