Monday, September 2, 2013

Bale Ndani ya Real Madrid Leo Hii

Hatimaye Gareth Bale amejiunga rasmi na Real Madrid ya Uhispania kwa kuvunja rekodi iliyowekwa na Cristiano Ronaldo.   Jumatatu ya leo imekua ya furaha kubwa ndani ya Jiji la Real Madrid mara baada ya kuwasili kwa mchezaji ghali duniani Gareth Bale akitokea club ya Tottenham ya nhini Uingereza. Amekua mchezaji ghali duniani mara baada ya uhamisho wake kugharimu £86 million (€100 million) kwa mujibu wa Tottenham, ingawa Real Madrid wanadai ni kiasi cha €91million. 
Kiwango kilichotajwa na Real Madrid kinaonekana kuwa ni kwaajili ya kukwepesha ukweli wa rekodi iliyovunjwa na Gareth Bale, ili rekodi ya Cristiano Ronaldo ionekane haijavunjwa bado. Ila ukweli ni kwamba Bale kaivunja rekodi hiyo na ndie mchezaji ghali zaidi duniani kwa sasa.  

PICHA MBALIMBALI ZA DIAMOND KATIKA NYIMBO YAKE MPYA YA NUMBER ONE

Msanii wa kizazi kipya Naseeb Abdul aka Diamond Platinum jana alizindua video ya wimbo wake mpya 'Number One' kwenye hoteli ya kifahari 'Serena Hotel' iliyopo jijini Dar es Salaam.









Add caption

Thursday, August 29, 2013

Msanii Wa Filamu Anusurika Kifo

MSANII wa filamu za Kibongo, Prisca Tadei hivi karibuni alinusurika kifo baada ya kupata ajali mbaya ya pikipiki wakati alipokuwa akielekea ‘location’ kushuti.









Mariamu Athuman ‘Kalunde’ alisema anamshukuru Mungu kwa kuwa msanii wake huyo mpaka sasa anapumua na anaonesha matumaini kwani ilikuwa ajali mbaya.













Ajali hiyo ilitokea wiki iliyopita maeneo ya Mbagala, jijini Dar ambapo Prisca aliumia vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake baada ya pikipiki aliyokuwa amepanda kugongwa na gari ambapo alikimbizwa Hospitali ya Mnazi Mmoja na kulazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu.






Homa la Pambano la Mabondia Cheka na Phil Williams lazidi Kupamba Moto

Bondia wa Marekani `Phil Williams` Atua Dar Kumkabili bondia wa Tanzania Francis Cheka siku ya kesho katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar Es Salaam

Wednesday, August 28, 2013

Jana mchana mwanadada Elizabeth Michael alifanya shopping maalumu ya nguo na vitu vingine kwa ajili ya uzinduzi wa filamu yake mpya ya Foolish Age inayotarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho kwenye ukumbi wa mlimani city jijini Dar es Salaam.

Uzinduzi wa filamu hii ambayo lulu mwenyewe anasema kuwa itakuwa ya kihistoria na aina yake utasindikizwa na wasanii mbalimbali wa kizazi kipya akiwema mwanadada Lady Jay dee.
Baada ya shopping hiyo mwanadada lulu pamoja na mama yake mzazi walipata nafasi ya kufanya mahojiano na kituo cha luninga cha DTV yote ni katika kuizungumzia filamu hii mpya inayotarajiwa kutingisha soko la filamu Tanzania

Hood lagonga mmoja,15 majeruhi

Mtu mmoja amefariki dunia na 15  wamejeruhiwa baada ya basi  la Kampuni ya Hood  likitokea kilombero kwenda jijini  Dar es salaamkumgonga  mtembea kwa miguu na kisha kuacha njia na kupinduka katika eneo la Kiembeni  Mikese Mkoani  Morogoro.
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Morogoro  Bonifasi Mbao  akizungumza kwenye  eneo la tukio amesema chanzo cha ajali  hiyo ni mwendo kasi ambapo dereva wa basi  gari  ilimshinda na kugonga mtembea kwa miguu na kisha kupinduka ambapo  dereva wa basi amekimbia mara baada ya tukio la ajali
Taarifa za  madaktari  katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro  zimeeleza  majeruhi wanaendelea na matibabu na mwili wa marehemu umehifahiwa katika chumba cha maiti hospitali ya mkoa wa morogoro .

KING CRAZY GK ARUDI TENA